Harmonize anapanga kuchora tattoo ya sura ya binti huyo kutoka Rwanda anayejulikana kama Phiona, almaarufu Yolo the Queen.
Mwimbaji gwiji Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize hatimaye amepata mpenzi mwingine baada ya kuachana na Fridah Kajala.
Mlimbwende anayeulikana kama Phiona, almaarufu Yolo the Queen ndiye aliyeuteka moyo wa supastaa huyo.
Akimtambulisha kwa mashabiki wake, Harmonize alisema wamekuwa wakionana na Phiona ‘chini ya maji’ kwa muda wa miaka mine.
Mwimbaji huyo alimsifia Phiona kama “aliyewazidi wapenzi wake wote wa awali” katika kile kilichoonekana kama kumpiga vijembe mpenzi wake wa zamani Kajala.
Aidha, mwimbaji huyo alisema kuwa anapanga kununua nyumba Kigali ili kuwa karibu na Phiona the Queen.
“ Ni vigumu sana kumjua anayekupenda kwa kweli unapokuwa na pesa na umaarufu. Nimekuwa tukizungumza na Phiona kwa zaidi ya miaka minne. Nahisi ni wakati wa kukuonyesha kuwa mie ni mwanamume kamili umefika”
“ Nakupenda kutoka kilindi cha moyo wangu @Yolo_the_queen. Wewe umewazidi wapenzi wangu wote wa zamani. Umenifanya kuhisi kana kwamba mimi ni Mrundi. Nitanunua nyumba Kigali ili niwe karibu na wewe,” Harmonize alisema.
Mwezi Aprili mwaka huu, Harmonize alisema kuwa ameificha tattoo ya Kajala na ile ya mlima Kilimanjaro.
HABARI NYINGINE: Tabia 28 Ambazo Zitakuheshimisha Kama Mwanamume
Wakiwa bado wanadeti, Harmonize alifanya tattoo ya Kajala ila akaitoa miezi mitano baadaye.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa murwa ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia info@gotta.news.