Hivi karibuni nimepatana na gumzo mtandaoni ambapo wanaume walikuwa wakichambua suala la shepu ya wanawake magwiji kitandani.
Hivyo, nilifuatilia gumzo hilo na maoni na kusema kweli niliishia kucheka huku nikiwaza: Kwani sisi wanaume huwaza ngono kutwa kucha?
Keshoye nilipitia gumzo linginge linaotawaliwa na wanawake na hapo pia nilijionea mambo.
Yaani mabinti wanaojifanya wapole huku nje wana ujuzi wa kuwatambua wanaume magwiji kitandani.
Binti mmoja kasema yeye huangalia vidole na saizi ya kiatu. Mwingine kasema anaangalia ukubwa wa pua kujua iwapo mechi itanoga ama itatumbukia nyongo.
Mwingine kasema anaangalia upana wa kifua na mwingine kasema kuhusu jinsi ya kupiga mswaki. haa! Acha nikomee hapo maana mabinti wana mambo.
Hii leo ni vizuri nisimulie waliyosema wanaume katika gumzo lile.
Kulingana na wanaume hao, wanawake walio na umbo la nambari nane la wastani na kiuno mithili ya nyigu ndio magwiji wa kunogesha mechi.
Baadhi ya wanaume walionekana kukubaliana kuwa mapenzi ya kisasa ni “nifanye, nikufanye” na wala sio mwanaume kujituma muda wote wakati wa mechi.
“Wao wana viuno vyepesi na ikiwa ni kwenda kasi, basi wapo,” alisema bwana mmoja.
Mabinti wa umbo nambari nane wastani pia walisifiwa kwa kuwa hawahemi haraka na hivyo mwanaume anayetaka kurina asali na kuheshimika lazima ajitume.
“Hawahemi haraka na iwapo wamtaka binti wa sampuli hiyo lazima uwe tayari kwa mapambano,” alisema mwingine.
Yote tisa, paliibuka jamaa mmoja aliyebadilisha mwelekeo wa gumzo hilo baada ya kuleta hoja iliyoungwa mkono na wengi.
Kwanza akawauliza wenzake? “Ni nani amewahi kuwa na mpenzi aliye na mwanya?”
Majibu yaliyoibuka pale yalikuwa ya kusisimua.
Hapo jamaa akatokea na kuwanyamazisha wenzake akiwaambia “waache mchezo maana utamu uliopo hapo kwa mwanya..acha tu…”
Mwengine aliwataja mabinti wenye mwanya kama ambao ni warembo na hawabahatishi kitandani.
“Hao ni moto wa kuotea mbali,” akasema mwingine.
Katika hali hiyo, yule bwana aliyeleta mada ya mwanya alirejea na picha ya binti mwenye umbo namba nane wastani…
Sekunde chache baada ya kuipakia pale..niliona jamaa wakisema.. weh, ule utamu uko hapo.
Mara ya kwanza sikuelewa kwa nini jamaa walimmiminia sifa kede kede yule binti mpaka jamaa mmoja alipoamua kutufafanulia sisi ambao tulikuwa bado hatushiki mita.
“Unaona hiyo nafasi iliyoko juu na mapaja ukikaribia kiuno…hiyo ni mambo yote” alisema yule bwana na hapo tukanfunguka macho.
Kulingana na wataalam wa mahaba, mabinti walio na umbo hilo ni wachache na ni nadra sana kuwapata.
HABARI NYINGINE: Yolo the Queen: Picha 10 za Mpenzi Mpya wa Harmonize
Hii hapa picha iliyopakiwa na jamaa huyo akiwasifia mabinti wenye shepu maalum kati kati ya mapaja.
Je, unayo taarifa murwa ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia info@gotta.news.