– Claudia Mselle amewaacha wanamitandao wengi vinywa wazi kwa shepu yake ya kupendeza
-Mselle ni afisa wa cheo cha Inspekta katika Jeshi la Polisi Tanzania
Umbo la Claudia Mselle limezua gumzo mtandaoni huku wanamitandao wengi wakimmiminia sifa askari huyo wa kike.
Picha za Inspekta huyo wa polisi akiwa amevalia magwanda ya kazi zimevutia maoni mengi huku wengi wakiusifia urembo wa askari huyo.
Aidha, Mselle, amejaliwa macho ya kupenza na tabasamu la kutuliza nyoyo.
Ripoti za vyombo vya habari zinaashiria kuwa Claudia Mselle anafanya kazi katika Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Kipolisi Rufiji.
Afisa huyo wa polisi amezuru vyombo vya habari kadhaa haswa redio kuzungumzia ukatili wa Kingono na migogoro ya ndani ya familia.
“Tumejipanga vizuri, katika kutoa ushauri kwa wababa na wamama kuja kutoa taarifa hizo kwani wivu wa kimapenzi ndo umekuwa chanzo cha kesi za mauaji, Msikubali kuacha familia zenu zikiwa yatima zikiteseka kwa ajili ya kukaa na kitu moyoni wakati Jeshi la Polisi lipo kwa ajili yenu kuja kutoa taarifa za unyanyasaji wa aina yoyote,” alisema hivi majuzi katika mazungumzo ya redio.
Vilevile, Claudia pia aliwarai wanaodhulumiwa kuripoti visa hivyo kwa polisi.
Mselle amekuwa akihudhuria ibada za kanisa kutoa elimu ya wajibu wa kanisa katika malezi na makuzi ya watoto.
Mselle pia katika vikao husisitiza umuhimu wa watoto kuinukia katika mandhari ya mapenzi.
Baada ya picha za Mselle kusambaa mtandaoni, wengi wa wanaume walifanya utani wakisema wangetaka kukamatwa na askari mrembo kama Claudia.
“Iwapo askari polisi wamekuwa warembo kiasi hiki, basi naomba kukamatwa,” alisema mmoja wa wanamitandao.
Hata hivyo, mmoja wa wanamitandao kutoka Tanzania alisema kuwa Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi vimesheheni warembo.
“Kuna warembo wengi katika Jeshi la Polisi na lile la Ulinzi. Ila Claudia amepata umaarufu mwingi kutokana na kazi anayoifanya,” alisema.
HABARI NYINGINE: Roxsana Diaz: Picha 10 za Mwalimu MREMBO Zaidi Duniani
Awali Kiswahili.GOTTA.news ilichapisha ripoti kuhusu jinsi wanaume wanavyopendezwa na wanawake wenye makalio makubwa.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa murwa ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia info@gotta.news.
