Habari

Rais Samia Suluhu Ashangazwa Wakenya Husema ‘Kuweka Kidole’ Kumaanisha Kutia Saini Mkataba

samia-suluhu-photos

– Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu ndiye wa hivi karibuni kuwatania Wakenya kuhusu Kiswahili chao ‘kibovu’

Kwa muda sasa, kumekuwa na gumzo mtandaoni kuhusu aina ya lugha ya Kiswahili inayozungumzwa Kenya.

Aidha, Watanzania, wanatatizika pakubwa kuelewa Kiswahili kinachozungumzwa Kenya, haswa Nairobi na nyanda za juu.

Ni wazi kuwa Kiswahili kinachozungumzwa pwani ya Kenya kinaeleweka vizuri na kinakaribiana na cha Tanzania.

“Hawa Wakenya hawa. Kwenda kusaini mkataba wanasema kuweka kidole mkataba,” alisema Rais Samia Suluhu huku akitabasamu.

Kiswahili.gotta.news imeng’amua kuwa msemo kuweka kidole unamaanisha mambo tofauti kabisa Tanzania.

Rais Samia Suluhu pia alisema, japo kwa utani, kuwa Watanzania wanajukumika kuwafunza Wakenya Kiswahili sanifu.

Samia Suluhu alikuwa akizungumza katika kongamano la 13 kuhusu Mifumo ya Chakula Afrika linalofanyika Dar es Salaam.

Rais wa Kenya William Ruto anayehudhuria kongamano hilo alikubali kuwa Watanzania ni magwiji wa lugha ya Kiswahili Afrika mashariki.

“Inajulikana kuwa Mtanzania akitaka kumshinda Mkenya katika mjadala ataendesha mjadala kwa Kiswahili,” alisema Rais Ruto.

Mwanahabari wa CNN Larry Madowo ambaye ana chimbuko lake nchini Kenya alisema kuwa Kenya na Tanzania ni ndugu.

“Sisi (Wakenya) tunaongea Kiswahili finyu na Watanzania ilhali nao wanatujibu na Kizungu (Kiingreza) kibovu.”

Konganamo hilo linanuiwa kujadili masuala kuhusiana na ubunifu, uendelevu na ukuzaji wa chakula.

HABARI NYINGINE: Claudia Mselle: Kutana na Afisa wa Polisi ambaye Figa yake ni Gumzo Mtandaoni

Rais Suluhu ndiye mwenyeji wa kongamano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa murwa ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected].

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Kali Zaidi

To Top
Sorry this site disable right click
Sorry this site disable selection
Sorry this site is not allow cut.
Sorry this site is not allow copy.
Sorry this site is not allow paste.
Sorry this site is not allow to inspect element.
Sorry this site is not allow to view source.