Watu na maoni

Tabia 28 Ambazo Zitakuheshimisha Kama Mwanamume

mwanaume

Hivi majuzi wanamtandao wameshiriki tabia 28 ambazo zinazomfanya mwanaume kuheshimika. Hii hapa orodha iliyotayarishwa na ripota wetu.

1. Ukiahidi timiza.

2. Usimwibe mke wa mtu.

3. Usijivune kuhusu hela ulizo nazo au kazi yako.

4. Usipende kujitokeza kama kimbelembele kwa kadamnasi. Watu hawapendi mtu wa kimbelembele.

5. Ukipata pesa nyingi wekeza, maana siku ya ukame itakuja.

6. Ukipata nafasi ya kuzungumza mbele ya watu hakikisha unasema machache.

7. Jifunze lugha ya unayetaka msaada kutoka kwake. Kwa mfano kama unayetafuta msaada kutoka kwake ni Mjaluo, jifunze maneno kadhaa ya Kiluo na kisha yaseme wakati mwafaka kwenye mazungumzo. Mwenyeji wako atafurahia.

8. Kuwa shujaa na hakikisha unawalinda wanawake na watoto wanaukutegemea. Usikubali mtu yeyote adhulumiwe ukiona.

9. Ukiona mtu amesisitiza mtazamo fulani wakati wa mazungumzo au mjadala, jaribu ubadilishe hoja pasi kumtukana.

10. Wafunze wanao umuhimu wa kuwajibika na kufanya bidii maishani.

11. Mche Mwenyezi-Mungu kwa kweli na na usiogope kukiri Imani yako katika sehemu za kuabudu kama kanisa na misikiti.

12. Mkeo akikukosea, mrekebishe kwa upendo na kwa kumwonyesha faida ya kubadilika.

13. Wachunge wazazi wako maana hutokuwa nao milele. Hakikisha wazazi wako hawakosi mahitaji ya kimsingi.

14. Waheshimu viongozi walio mamlakani ila usiogope kuwakosoa wanapokosa.

15. Epuka tabia ya kuonyesha utajiri hadharani au kujivuna jinsi ulivyofanikiwa.

16. Kuwa na nafasi ya kuketi pekee yako na kuchukua hesabu ya mafanikio na matokeo yasiyofaa yanayotokana na maamuzi yako.

17. Saidia pasi kutarajia msaada.

18. Hakikisha unachunga afya yako kwa kuzingatia lishe bora na kufanya mazoezi.

19. Epuka watu walio kiburi na wanaopenda kujisifu jinsi walivyo na wanawake wengi.

20. hakikisha unamzawadi mkeo na kumpenda na usiwahi kumkweza juu ya mwanamke mwingine.

21. Epuka umaarufu wa mitandaoni na kujipendekeza kwa watu wasiokujua wala wasiojua ndoto na machungu yako.

22. Usiogope kuchukiwa au hata kubezwa haswa unaposimamia haki.

23. Usifanye mambo yanayokinzana na dhamiri yako.

24. Epuka unywaji wa pombe kupindukia. Ukiweza epuka pombe kabisa.

25. Usimwonee wivu mtu yeyote. Bali jitume ufanye bidii na utafanikiwa.

26. Wasaidie wakongwe, walemavu, wagonjwa na watoto kuvuka barabara. Mwanaume ni kiongozi.

27. usimwambie yeyote maneno ambayo yanaweza kumfanya ajidharau au kujihisi hana dhamani.

28. Sisitiza kula wa mwisho katika sherehe am ahata kwako nyumbani baada ya kila mtu amepatiwa mgao wake.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa murwa ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected].

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Kali Zaidi

To Top
Sorry this site disable right click
Sorry this site disable selection
Sorry this site is not allow cut.
Sorry this site is not allow copy.
Sorry this site is not allow paste.
Sorry this site is not allow to inspect element.
Sorry this site is not allow to view source.