Burudani

Iweje Mwenye ‘Udongo’ Ajiamini Kuliko Aliye na Digrii?

udongo

Hivi karibuni, mwimbaji gwiji Harmonize amezua gumzo kwenye mitandao jamii nchini Kenya na Tanzania kuhusu wanaume kupendezwa na wanawake waliojaliwa “udongo”.

Hii ni baada ya kuweka wazi kuwa yuko katika uhusiano na mlimbwende Yolo the Queen kutoka Rwanda.

Yolo the Queen amejaliwa udongo na wanamtandao wa Kenya na Tanzania, wamekuwa wakimtania Harmonize, “kuwa karogwa na mabinti wenye nyash kubwa.”

Kilichofuata ni utani mtandaoni huku wanamtandao wakitoa maoni kwenye picha za mabinti waliojaliwa udongo kuwa, ‘hakikisha Harmonize asimwone!’

Kulingana na wanamitandao hao, Harmonize hawezi kujizuia kumwandama mwanamke aliyejaliwa udongo.

Patrick ambaye ni mwanahabari katika mojawapo ya vituo maarufu Kenya anasimulia jinsi wanaume wanavyojisahau wanapopatana na mwanamke aliyejaliwa udongo na shepu ya kuvutia.

“Tulikuwa watatu na kampuni ilitaka kumpandisha cheo mmoja wetu na kisha ahamishwe kwenda Nairobi,” asimulia Patrick huku akitabasamu.

“Msimamizi wetu na mkuu wa kitengo alikuwa jamaa aliyependa mabinti sana. Hivyo nilijua singetoboa mchujo. Wenzangu wawili ambao walikuwa mabinti warembo walikuwa kwa nafasi nzuri zaidi,” alielezea Patrick.

Mwanahabari huyo anadai kilichofuata kilimfanya kusadiki kuwa udongo una uwezo wa kumpaisha mwanamke.

“Kusema ukweli, kati ya mabinti hao wawili, aliyekuwa ‘amekauka’ alikuwa mwandishi bora kuliko mwenzake aliyejaliwa udongo vizuri.”

“Nakumbuka jinsi bosi wetu wa Nairobi alivyozuru afisi zetu Mombasa na kuwakagua wote wawili. Nakumbuka akimwangalia yule binti aliyejaliwa udongo huku akimeza mate na baadaye kutoa kauli yake, ‘huyu ni mwandishi bora na naona ataandika habari nzuri zitakazofurahisha wasomaji wetu’” asema Patrick huku akicheka hadi kutokwa machozi.

Anadai uamuzi huo wa bosi wao kutoka Nairobi uliwaudhi mno wafanyakazi wengine ambao walimkemea kisiri bosi wao kwa kuendeleza mfumo wa kipendeleo.

“Hatimaye binti ‘aliyekauka’ aliacha kazi ya uanahabari na kuingilia ualimu. Hii leo, mimi na rafiki zangu hutumia msemo, ‘ni mwandishi mzuri’ kumaanisha ni mrembo na amejaliwa udongo,” asema Patrick.

Amina, binti kutoka Mombasa anasema kuwa mambo yake yalienda upogo siku aliyotoa buibui wakati wa ‘team building’ na wanaume kuona shepu yake.

“Kutoka siku hiyo, wafanyakazi wenzangu, wengi ambao ni wanaume walianza kuniandama “inbox” wakisema walikuwa tayari kunipatia chochote nilichotaka ili kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mimi,” asema Amina.

“Wanaume ni viumbe wanaovutiwa zaidi na wanachokiona na hivyo hainishangazi wanafurahishwa na wanawake waliojaliwa udongo. Ushawaona wanavyokodoa macho wanapokutana na mabinti wenye makalio makubwa?” asema Amina.

Amina anadai mmoja wa mabosi wake aliahidi kumnunulia nyumba Nyali iwapo angekubali kuwa mke wa pili.

“Nilikataa maana niliona itakuwa kujidhalilisha,” asema Amina.

Yolo the queen

Mpenzi wa Harmonize Yolo the Queen. Photo/courtesy

Sawia na Amina, Jackline anaamini wanaume Waafrika wanapendezwa zaidi na wanawake waliojaliwa udongo.

“Wanabiashara na mafundi wa nguo za wanawake wanajua wanaume ni watu wenye tamaa na hivyo wanakuja na fashoni zinazosisitiza ukubwa na shepu ya makalio,” asema Jackline.

Na je, ni kila mwanamume anayedondokwa na mate anapomwona mwanamke aliyejaliwa udongo?

“Mimi si shabiki wa makalio makubwa. Napenda saizi wastani,” Asema Benjamin Omondi.

Omondi anasema kuwa zamani alipendelea mabinti wanene ila sasa anapendelea wastani ambao wanaweza kwenda kasi.

“Kisha kusema ukweli, waliojaliwa udongo huishia kuhema haraka ikifika wakati wa mechi,” asema Omondi.

Samuel Waithaka kwa upande wake alisema hawezi deti mwanamke asiye nyash.

HABARI NYINGINE: Yolo the Queen: Picha 10 za Mpenzi Mpya wa Harmonize

“Kwangu mie mwanamke kuwa na nyash kubwa ni lazima. Ni sawia na serikali inapotangaza nafasi za kazi na kusisitiza walio na digrii ndio wanaostahili kutuma maombi” asema Waithaka.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa murwa ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected].

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Kali Zaidi

To Top
Sorry this site disable right click
Sorry this site disable selection
Sorry this site is not allow cut.
Sorry this site is not allow copy.
Sorry this site is not allow paste.
Sorry this site is not allow to inspect element.
Sorry this site is not allow to view source.