Watu na maoni

Tabia 17 Zinazokuzuia Kutajirika

jamaa-tajiri

James Kamau kutoka Mombasa, Kenya anashiriki mawaidha ambayo kwa mtazamo wake yanachangia pakubwa kutajirika ama kufeli kwa wanaume.

“Wewe sio mkakamavu na hauna ghera ya kutimiza malengo yako,” rafiki yangu aliniambia wakati mmoja tukiwa tumetulia kikao.

Basi ikanigusa moyo na baadaye nikiwa nimetulia peke yangu nikijiuliza kichocheo cha rafiki yangu kusema aliyoyasema.

Nilipotathmini, nikaona ni kweli nimekuwa nikiishi bila mpangilio na napenda burudani kuliko kuijenga kesho yangu.

Baadaye, nilijiandikia listi ya tabia zinazonifanya kutofanikiwa. Hebu itazame huenda ikakufaa pia.

1. Unapenda sana starehe na unapenda kufurahisha marafiki. Umefungua video You Tube unataka kuanza kujifunza ujuzi flani kisha unapokea simu ya rafikiyo akikuitia pombe. Wewe huwezi kukataa, na hivyo unaondoka mara moja kukutana na rafikiyo kustarehe. Na hivyo ndivyo unasahau kujifunza ujuzi huenda ingekuwa faida baadaye.

2. Una woga wa kujaribu na unaogopa kufeli. Hivyo wewe unapenda kukashifu maana hiyo ni rahisi. Ukiambiwa uanze biashara hautaki. Sababu? Eti maana hauwezi ama unajua biashara itaanguka. Kazi yako ni kubarizi tu wikendi ukilewa na kuangalia EPL.

3. Uko mitandao jamii ambako umejenga umaarufu wa kufurahisha wanamitandao haswa mabinti. Umepata sifa kedekede ila hauna kitu mfukoni. Ondoka mtandaoni uende ujitume.

4. Unatekeleza kazi za wenyewe kwa weledi na umakini ila hutaki kujituma katika kazi yako. Ni lazima ujue kufuata ndoto yako inahitaji kujitolea na kujikakamua.

5. Unapenda sifa za kipumbavu na kujipendekeza kwa watu. Hivyo unatumia hela nyingi kuwanunulia watu pombe ili ufanye urafiki nao.

6. Unaamini kazi ya kuandikwa na hauna mpango mbadala. Hii ni kwa sababu unaamini
utaandikwa milele. Siku utakayostaafu ama kufutwa kazi ndio utafahamu umuhimu wa
kuwekeza na kujenga biashara yako binafsi.

bajeti

Kuwa na bajeti kuna umuhimu katika kuhakikisha unatumia kiwango cha pesa zinazohitajika. Picha/mtandao

7. Una wanawake wengi na kazi yako ni kuwapa hela na kuwapeleka deti katika mikahawa ya kifahari. Mbona usioe uwache kufuja hela?

8. Hauna hamu ya kubadilisha maisha yako. Unaona magari na nyumba nzuri wavitamani ila hauna mpango wa kubidiika ili siku moja nawe umiliki unavyovitamani.

9. Unaishi maisha ya juu zaidi ya unavyoweza kumudu. Hivi una madeni ya kufanikisha starehe za kipuuzi kama unywaji wa pombe na dawa za kulevya.

10. Unapenda kushindana na wenzako. Ukiona mwenzako kazini kanunua gari nawe wachukua mkopo kununua gari jipya. Ukiona mwenzako ana simu kali basi wewe wakimbia kununua yako.

11. Hauna mtandao wa marafiki wa maana. Mtandao wako ni wanywaji pombe ambao siku ukiharibikiwa watakuacha. Hautaki kujiunga na vyama vya uwekezaji.

12. Umewatelekeza wazazi. Ukweli ni kuwa katika amri 10 za Mwenyezi-Mungu katika Biblia, ya tano kuhusu kuwatii wazazi ndiyo iliyo na ahadi. Unapowatelekeza wazazi, basi mioyo yao huwa inauma na kuungulika ndani kwa ndani.

13. Hauna subira. Waambiwa uanze biashara leo ili uvune matunda miaka kumi ijayo. La hasha, wasema ukijifariji kuwa hujui iwapo utafika huko. Kwa kifupi haja yako ni suluhu na faida za haraka haraka ambazo hazihitaji kungoja.

14. Hujazuru dunia. Kuzuru sehemu tofauti duniani husaidia pakubwa ‘kufungua’ macho na akili. Asiyezuru dunia hujiona mahiri na aliyefika. Aidha, ukizuru dunia utakutana na wawekezaji na nafasi za uwekezaji murwa ambazo zitakuwezesha kuzalisha mali.

15. Unavunjwa moyo na matatizo madogo na unaamini watu hufanikiwa kwa sababu wana ‘kismati’ na sio kwa sababu wana bidii.

16. Unapenda filamu za ngono na kujichua. Ukweli ni kwamba tabia hizi mbili zinakufyonza ubunifu na ari ya kujituma kazini.

HABARI NYINGINE: Tabia 28 Ambazo Zitakuheshimisha Kama Mwanamume

17. Huijali afya yako. Hufanyi mazoezi na unakula vyakula visvyorutubisha mwili na uwezo wa kufikiria.

READ ENGLISH VERSION

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Kali Zaidi

To Top
Sorry this site disable right click
Sorry this site disable selection
Sorry this site is not allow cut.
Sorry this site is not allow copy.
Sorry this site is not allow paste.
Sorry this site is not allow to inspect element.
Sorry this site is not allow to view source.